Habari

Huyu ndio balozi wa Italia auawa DR Congo kwenye msafara wa Umoja wa Mataifa (+ Video)

Wizara ya mambo ya nje ya Italia imesema kuwa balozi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameuawa katika shambulio dhidi ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo.

Balozi Luca Attanasio na mwanajeshi mmoja wa Italia wameuawa katika shambulio lililotokea karibu na mji wa Kanyamahoro

Dereva wa gari raia wa Congo pia aliuawa katika tukio hilo.

Maafisa katika mbuga ya wanyama ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara.

Makundi mengi yaliyojihami yanaendesha harakati zake karibu na mbuga hiyo inayopakana na Rwanda na Uganda.

Walinzi wa mbuga hiyo wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na kuuawa na waasi.

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba wizara ya mashauri ya kigeni inathibitisha, kifo leo, mjini Goma, cha balozi wa Italia ,” taarifa ya wizara ilisema.

Watu wengine walwili waliouliwa walikuwa ni askari polis mwenye umri wa miaka 30 Vittorio Iacovacci, ambaye amekuwa akihudumu katika ubalozi tangu mwezi septemba mwaja jana, na dereva wao raia wa Congo, ambaye jina lake bado halijatangazwa rasmi..

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi ametoa taarifa yake ya “rambi rambi kubwa”, huku Rais Sergio Mattarella akilaani “shambulio la uoga”.

Waziri wa mambo ya nje Luigi Di Maio ameelezea “kushitushwa sana na huzuni kubwa ” na mauaji ya “kikatili “

“Leo Italia inaomboleza vifo vya watoto wake wawili na inazikumbatia familia zao ,” alisema, na kuongeza kuwa : “Hakuna juhudi zitakazosazwa katika kutoa mwangaza juu ya nini kilichotokea .”

Ramani

Haijafahamika wazi ni nani aliyekuwa nyuma ya shambulio hilo, lakini makundi mengi yenye silaha yanafahamika kuendesha harakati zake ndani na maeneo yanayozingira mbuga ya wanyama ya Virunga.

Bw Attanasio alikuwa akisafiri kutoka Goma ambako alikwenda kuzulu “mradi wa shule ” katika kijiji cha Rutshuru mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ilisema taarifa ya shirika la WFP lenye makao yake Roma.

“Shambulio hilo …lilitokea katika barabaraambayo awali ilitangazwa kuwa huru kwa watu kusafiri bila walinzi ,”iliongeza.

Jeshi la DRC limepeleka wanajeshi kusaidia kusaka eneo hilo.

Bofya hapa chini kutazama zaidi.

https://www.instagram.com/tv/CLoIpwzhkq0/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents