FahamuHabariSiasa

Huyu ndio Kamanda mkuu wa Hamas auawa katika mashambulizi ya anga na Israel

Kamanda mkuu wa Hamas ameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) amesema.

Katika chapisho kwenye X, iliyoandikwa kwa Kiarabu, Avichay Adraee alisema Murad Abu Murad alihusika pakubwa katika shambulio la Israel Jumamosi iliyopita, ambalo liliua zaidi ya watu 1,300.

Hamas haijathibitisha kifo hicho.

Israel na Misri zasema raia wa Marekani huenda wakaondoka Gaza

Raia wa Marekani wataweza kuondoka Gaza kupitia mpaka wa Rafah kuelekea Misri, afisa wa Marekani anasema.

Kivuko hicho kitafunguliwa kuanzia saa 12:00 hadi 17:00 kwa saa za huko leo, kufuatia makubaliano kati ya serikali ya Israel na Misri.

Bado haijabainika iwapo Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, itawaruhusu raia wa Marekani kuondoka katika eneo hilo.

Zaidi ya 2,200 waliuawa na 8,700 kujeruhiwa huko Gaza – wizara

Takriban watu 2,215 wameuawa na 8,714 wamejeruhiwa huko Gaza, Wizara ya Afya ya Palestina imesema.

Katika Ukingo wa Magharibi, watu 54 waliuawa na 1,100 walijeruhiwa.

Darroch: Uingereza lazima iitake Israel kuongeza muda wa uokoaji

Lord Kim Darroch, balozi wa zamani wa Uingereza nchini Marekani na mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Uingereza, anasema ni lazima muda zaidi utolewe kwa Wagaza kuondoka kaskazini mwa eneo hilo ili kuepuka “janga la kibinadamu”.

Akizungumza na kipindi cha Today Radio 4, Lord Darroch alisema anafikiri mashambulizi ya ardhini ya Israel yenye lengo la kuwaondoa Hamas yatashindwa, wakati kizazi kijacho cha wapiganaji wa Kipalestina “tayari kimekuwa na itikadi kali”.

Bwana Darroch pia alisema ataishauri serikali ya Uingereza – ambayo imesisitiza uungaji mkono wake kwa Israel na imelaani mashambulizi yaliyoanzishwa na Hamas – kuhimiza kupunguza kasi ya dirisha la saa 24 kwa watu kuondoka kaskazini mwa Gaza.

Alisema pia atawataka mawaziri kuwaambia Israel “ifikirie kwa makini kuhusu operesheni hiyo”.

“Lakini mimi ni mgeni sasa,” anaongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents