Huyu ndio Samaki wa ajabu wa kale, aliyepatikana Afrika na kuishi miaka mingi zaidi

Samaki wa kale anayefahamika kama coelacanth anaweza kuishi kwa muda mrefu sana, hadi karne nzima, kulinga na utafiti mpya uliochapishwa na jarida la Current Biology.

Samaki huyu awali alifikiriwa kuwa alitoweka duniani kabla ya hatimaye kupatikana katika maji ya Afrika na Sulawesi kwa kipindi chote cha karne ya 20.

Katika tafiti za awali , coelacanths walikadiriwa kuwa na uwezo wa kuishi kwa miaka ipatayo 20. Lakini katika makadirio ya hivi karibuni, samaki hawa wanaweza kuishi kwa mamia ya miaka ndani ya bahari, sawa na papa.

Watafiri Wafaransa waliochunguza alama zilizopo kwenye masalia madogo ya samaki coelacanth yaliyotunzwa katika makumbusho walibaini ishara tatu za pete zinazoaminiwa kuonesha umri sawa na zile umri wa mti.

Watafiti wanaamini coelacanths wanaweza kuzaa tu wanapokuwa na umri wa kati wa maisha yao na wanaweza kuishi na mayai mwilini mwao kwa hadi miaka mitano.

Wafanyakazi wakimuingiza coelacanth ndani eneo la maonyesho
Wafanyakazi wakimuingiza coelacanth ndani eneo la maonyesho ya ‘Bahari katika Makumbusho ya Kitaifa ya asili mjini Paris, Machi 2019.

Kwasababu kwa asili yake huzaa vizazi vichache, ongezeko la taratibu la samaki hawa huwaweka katika hatari kubwa ya kutoweka.

Baadhi ya mambo ambayo yanafikiriwa kuchangia uwepo wake ni mabadiliko ya hali ya hewa na uvuvi wa kupindukia.

Kufahamu historia ya maisha ya coelacanth kunaweza kuwa msingi imara wa katika juhudi za uhifadhi wa samaki hawa, anasema msomi Bruno Ernande kutoka Chuo kikuu cha Montpellier, nchini Ufaransa.

” Mfumo muhimu sana wa uhifadhi wao ni uwezo wa kutathmini maeneo ya kiografia ya spishi hawa.

“Kwa taarifa mpya tutakuwa vyema kutathmini walipo ,” Ernande aliiambia BBC.

Coelacanths hupatikana katika maeneo ya mwambao wa Indonesia na bahari ya Hindi
Coelacanths hupatikana katika maeneo ya mwambao wa Indonesia na bahari ya Hindi

Kwa muda mrefu Coelacanth walidhani kuwa walitoweka hadi walipopatina hatimaye katika nyavu za wavuvi nchini Afrika Kusini mwaka 1938.

Makundi yao mawili baadaye yalipatikana yakiishi mbali kidogo ya mwambao wa Afrika mashariki na mbali kidogo ya mwambao wa Sulawesi.

 

Idadi yao katika Afrika imeainishwa kama iliyomo hatarini. Watafiti wanakadiria kwamba ni mamia kadhaa ya coelacanths waliosalia pale.

” Coelacanth wanaonekana kuwa ni spishi wanaoishi miaka mingi miongoni mwa viumbe wa majini, kama vile papa waishio katika kina kirefu cha maji na huishi takriban kilomita 1.8 chini ya kiwangi cha maji ya ya bahari ),” alisema Kelig Mahe kutoka taasisi ya utafiti wa masuala ya uvuvi ya Ufaransa ya North Sea Fisheries Research Unit kilichopo Boulogne.

“Matokeo yetu yanaonyesha kuwa samaki huyu anaweza kuwa hatarini kuliko ilivyowahi kufikiriwa kutokana na historia yake ya ajabu ya maisha.

” Taatifa hizi mpya kuhusu baiolojia na historia ya maisha ya coelacanth ni muhimu kwa uhifadhi na udhibiti wa viumbe hawa ,” Mahe alisema.

Wageni wakipita katika eneo anakohifadhiwa spishi wa coelacanth ambaye alikamatwa katika eneo la Manado bay mwaka 2007.
Wageni wakipita katika eneo anakohifadhiwa spishi wa coelacanth ambaye alikamatwa katika eneo la Manado bay mwaka 2007.

Samaki huyu alionyeshwa katika kituo kikubwa cha uhifadhi cha Grand Kawanua Convention Center wakati wa Mkutano wa dunia wa bahari tarehe 15 Mei 2009.

Katika tafiti zijazo, wanasayansi wanapana kumtathmini zaidi samaki huyu kubaini zaidi iwapo kiwango cha ukuaji wa spishi hawa kina uhusiano na joto

Majibu yatakayojitokeza yatatoa mwanagaza mpya katika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa spichi hawa waliomo hatarini.

Mababu wa coelacanth waliishi miaka milioni 420 iliyopita, wakahimili mabadiliko ya maumbile ya mabara na vimondo vilivyowamaliza dinosau.

Wakiishi katika mapango yaliyoko kwenye sakafu za bahari, coelacanth wanaweza kuku ana kufikia urefu wa mita 1.8, na uzito wa zaidi ya kilogramu 90.

Credit by BBC.

Related Articles

Back to top button