Habari
Huzuni Kifo cha Denis Sebo wa EFM na TV E

Mkurugenzi Mtendaji Wa #EFMnaTVE Bwana @majizzo Ametangaza Kifo Cha Aliyekuwa Mkurugenzi Wa Uendeshaji Na Biashara Bwana Denis Busulwa ( Ssebo ) 💔
Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram Ameandika👇
“Kwa moyo mzito na machozi mengi, nasikitika kutangaza kifo cha rafiki, kaka, aliyekuwa msimamizi wa ndoa yangu, na mfanyakazi mwenzangu aliyeitumikia EFM na TVE kwa nguvu zake zote, ndugu yangu Ssebo.
Ssebo amefariki usiku huu katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Kwa sasa mturuhusu kuaanda taratıbu zote zinazohusiana na msiba
huu wa Ghafla, ambao kwa kweli siwezi kuuelezea. Taarifa zaidi tutazitoa baadae.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.”





