Michezo

‘I am the BEST’, Mo Salah kwa msisitizo adai hakuna anayemfikia

Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah amedai kuwa yeye ndiye ‘bora’ zaidi kuliko mchezaji yeyote katika nafasi yake na kusisitiza kuwa anawashinda wapinzani wake katika takwimu.

 

Mshambuliaji huyo wa Misri alitajwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa FWA 2022 baada ya msimu mwingine wa kuvutia ndani ya kikosi cha Jurgen Klopp.

Licha ya kushuka kiwango katika wiki za hivi karibuni, lakini fanikiwa kufunga jumla ya magoli 30 katika mechi 48 za mashindano yote hadi sasa msimu huu na kwa sasa anaongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania kiatu cha dhahabu.

Salah mwenye umri wa miaka 29 amekubali kiwango chake msimu huu na kuamini kuwa kinastahili tuzo hiyo ya 2022 FWA Footballer of the Year kwani anaidai ni bora kuliko mchezaji mwingine yeyote katika nafasi yake – ikiwa ni pamoja na wachezaji wenzake Sadio Mane, Diogo Jota na Luis Diaz.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents