Habari

Idadi ya watu duniani kufikia bilioni 8, Novemba 15

Idadi ya watu duniani itafikia bilioni 8 tarehe 15 Novemba, Umoja wa mataifa umesema Jumatatu, huku India ikiipiku China kama taifa lenye watu wengi zaidi ulimwenguni.

Umoja wa mataifa ulitoa ripoti yake kuhusu matarajio ya idadi ya watu ulimwenguni mwaka wa 2022, katika siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani, ambayo inaadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Julai.

Kauli mbiyu ya mwaka huu ni “ Ulimwengu wa bilioni 8, kuelekea mustakabali thabiti kwa wote, kutumia fursa na kuhakikisha haki na maamuzi binafsi kwa wote.”

Licha ya kuwa mwaka wa 2022 waonekana kuwa mwaka ambapo idadi ya watu imeongezeka zaidi duniani, kwa mujibu wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres, ongezeko la watu lilipungua chini ya asilimia 1 mwaka wa 2020, ikiwa ni ongezeko ndogo zaidi tangu mwaka wa 1950.

Umoja wa mataifa unasema kuna uwezekano idadi ya watu ulimwenguni ikafikia bilioni 8.5 mwaka wa 2030, bilioni 9.7 mwaka wa 2050 na kufikia bilioni 10.4 ifikapo mwaka wa 2080.

Idadi ya watu inatarajiwa kubaki bilioni 10.4 hadi mwaka wa 2100.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents