Habari

Idadi ya watu duniani yafikia bilioni nane

Idadi ya watu duniani inakadiriwa kufikia watu bilioni 8 hii leo huku sehemu kubwa ya ongezeko la watu linashuhudiwa kwenye mataifa yanayoendelea hususani barani Afrika.

Siku ya leo Jumanne ndiyo ilichaguliwa na Umoja wa Mataifa kama tarehe ya ishara ya kufikiwa kwa idadi hiyo ya watu bilioni 8 ulimwenguni ambayo makadirio yake yanatokana na takwimu za kisayansi.

Nigeria, Tanzania, Ethiopia na Congo ni miongoni mwa mataifa 8 ambayo Umoja wa Mataifa unasema yatakuwa nyumbani kwa nusu ya ongezeko la idadi ya watu ulimwenguni kati ya mwaka 2022 hadi 2050.

Nchini nyingine ziitakazochangia ongezeko la watu ulimwenguni ni pamoja na Misiri, Pakistan, Ufilipino na India. Watunga sera wa kimataifa wana wasiwasi kuwa idadi ya watu itaongeza mzigo kwa serikali nyingi duniani ikiwa ni pamoja na barani Afrika ambako huduma muhimu za jamii bado hazipatikani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents