
Kulingana na uchunguzi wa kitaifa uliofanywa na Advanced Dermatology kutoka Illinois, Marekani umebaini kuwa idadi ya wanaochukia tattoo walizochora yaongezeka.
Katika uchunguzi huo uliofanywa kwa kipindi cha mwaka mmoja ulibaini kuwa idadi ya waliotaka kufuta tattoo zao imefikia asilimia 51 ikiipiku idadi ya awali ikiwa asilimia 15.
Aidha Dk. Alissa Lamoureaux Daktari wa ngozi aliyeidhinishwa na bodi huko Shrewsbury alieleza kuwa watu hutaka kuondolewa tattoo zao kutokana na Umri wao kwenda.
“Ni watu wa Umri kuanzia 30-40 huwenda waliochora Tattoo hizo wakiwa wadogo na sasa wanaona ni kama fashioni hiyo imepitwa na wakati katika umri wao” amesema Dk Alissa.
Vipi bado una Mapenzi na Tattoo yako, au na wewe upo kwenye mstari wa kutaka kuifuta??