Burudani

IDRIS SULTAN BADO YUPO MATATANI: Jalada la uchunguzi tuhuma zinazomkabili latua kwa DPP

Jalada la uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili msanii wa vichekesho nchini Tanzania, Idris Sultan limepelekwa ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Hayo yameelezwa leo Jumatano Novemba 13, 2019 na Benedict Ishabakaki ambaye ni mwanasheria wa msanii huyo.

Idris anadaiwa kusambaza habari za uongo chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao na kujifanya Rais chini ya kifungu cha 15 cha makosa ya mtandao.

Ijumaa Novemba Mosi, 2019 Idris aliripoti kituo cha polisi kati baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Makonda alichukua uamuzi huo baada ya msanii huyo kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa.

Pia, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents