Uncategorized

Ifahamu ratiba kamili ya majeruhi wa Lucky Vincent wanaoenda Marekani asubuhi hii

Baada ya ajali mbaya iliyohusisha watoto wa shule ya Lucky Vincent Karatu, Jumamosi iliyopita, majeruhi waliopona katika ajali hiyo, watoto watatu, pamoja na familia Zao, wanatarajia kuondoka nchini asubuhi hii, wakielekea Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi.


Kwa mujibu wa Mbunge wa Singida kaskazini, mheshimiwa Lazaro Nyalandu, ambaye anasimamia safari hiyo, amesema watoto hao wataambatana na madaktari wawili pamoja na wazazi wao.

Majeruhi hao wanatarajia kuagwa kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, KIA, na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Ndege inayowachukua majeruhi hao ilitumwa maalum na taasisi ya Samaritan Purse ya huko nchini Marekani, ambapo imewasili Jana usiku ikiwa yenye maandhari ya hospitali ndani yake na ndio itakayowafikisha Marekani Kwenye matibabu.


Ripoti zimesema kwamba taasisi hiyo imejitolea kuwasafirisha na kuwahi matibabu bure, majeruhi hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents