Ifahamu Simu mpya ya Infinix yenye uwezo wa kujikunja mara tatu

Infinix inakaribia kuzindua toleo jipya la simu itayofahamika kwa jina la Infinix ZERO Flip Min Tri-Fold yenye uwezo wa kujikunja mara tatu na yenye ukubwa sawa na simu ya kawaida pindi inapokunjuliwa.
Simu hii inakwenda kuwa kimbilio kwa vijana wengi wanaopenda simu za kisasa na zenye uwezo wa kuwa na mionekano mingi bila kushuka kwa ufanisi haswa wakati wa uchukuaji wa video ama Picha.
Infinix kupitia taarifa yao wameeleza kwamba simu hii itakuwa na uwezo wa kutumika katika mazingira mengi ikiwemo kwa watu wanaopanda milima kuweza kuininginiza kwenye nguo na kuchukua picha/video na pia inaweza kutumika kama Camera maalumu ya kuchukulia matukio wakati wa ufanyaji wa mazoezi (Gym) ama kwa kuning’iniza ndani ya kioo cha Gari na kuchukua video na picha pindi linapokuwa barabarani.
Toleo hili bado halijapangiwa muda wa kutoka hivyo linabaki kuwa kama mfano wa namna siku zijazo teknolojia hii itavyokwenda kuteka soko na mioyo ya watumiaji wa simu kote Duniani haswa Infinix.
Kwa mawasiliano zaidi tembelea kurasa zetu za kijamii @infinixmobileTz au piga simu +255760552543