Technology

Ifahamu simu yenye Kamera ya maajabu inayokimbiza sokoni kwasasa duniani

Infinix S5 Pro ni moja kati ya simu bora zaidi yenye bei nafuu katika soko la simu janja Tanzania kwa sasa, ambapo tangu kuzinduliwa kwake rasmi Machi 6 mwaka huu, imezua gumzo kutokana na ubora wake wa kipekee ambao leo tutauchambua hapa.


Simu hizi zina RAM zenye ukubwa tofauti wa 4GB na 6GB hivyo itakuwezesha kufungua programu au kufanya mambo mbalimbali kwa wakati mmoja bila kukwama kwama, na uwezo wake wa kuhifadhi taarifa (video, picha, miziki, faili) ni 64GB na 128GB.

Aidha, ina sehemu ya kuweka memory card kwa ajili ya kuiongezea uwezo wa kuhifadhi taarifa.

Kwa wale wanaopenda simu zenye kioo kikubwa na chenye ubora simu hii yenye uzito wa gramu 195 ni kwa ajili yao kwani kioo chake (IPS LCD) kina ukubwa wa inchi 6.53″ chenye ubora wa 1080p.

Kamera yake ya mbele (selfie camera) yenye 40MP ni ya kipekee zaidi ambapo hutokezea juu ya simu pale unapotaka kupiga picha na ukimaliza inarudi kujificha ndani ya simu, (mechanical pop-up piece) hii inakuwezesha kupata picha zenye ubora zaidi.

Wale wapiga picha, simu hii ina kamera 3 za nyuma ambapo kamera ya kwanza ina 48MP (f/1.8 lens), kamera nyingine ina 2MP ambayo hii ni sensor kwa ajili ya picha za karibu (potraits) ambazo huonesha hadi sehemu ya mabega.

Kamera ya mwisho (QVGA) ni maalum kwa ajili ya kuweka sawa mwanga wakati wa upigaji picha. Pia inauwezo wa kurekodi video zenye ubora na muonekano ang’avu wa hadi 1080p.

Yote haya ni kuhakikisha wewe mtumiaji unapata kilicho bora zaidi.

Uwezo wa betri ya simu hii ni 4,000 mAh ambayo inaweza kukaa zaidi ya siku moja bila kuichaji. Simu hii ina mfumo endeshi (OS) Android 10, na utaweza kuuboresha kadiri maboresho yatakavyotoka.

Katika kuhakikisha kuwa unapata habari mahali popote ulipo, ndani ya simu kuna programu ya redio (FM Radio).

Jingine ni kwamba wameimarisha usalama wa taarifa zako kwani utaweza kuifunga simu yako kwa kutumia alama za kidole.

Hata hapa Bongo unaweza kuipata simu hii tembelea maduka ya Infinix yaliyopo karibu nawe nchi nzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents