Burudani

Ikiwa ni siku mbili zimepita tangu waachie album ya ‘Everything is Love’, Jay-Z apata shavu lingine kubwa

Ikiwa ni siku mbili zimepita tangu Jay-Z na mkewe Beyonce waachie album yao ya pamoja ya “Everything is Love” ambayo hadi sasa inafanya vizuri kwenye soko, hatimaye Mr. Carter amekwara dili lingine kubwa.

Jay-Z

Jay-Z mapema jana usiku ametangazwa rasmi kuwa Afisa Ubunifu na Ushauri wa kampuni ya mavazi ya PUMA kwenye kitengo cha mpira wa kikapu.

Taarifa za awali zilizotolewa na mitandao mingi nchini Marekani zilieleza kuwa Jay Z amechaguliwa kuwa Rais lakini baadaye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Adam Petrick alikuja kutoa taarifa rasmi kuhusu dili hilo.

Ninaweza kuthibitisha kuwa kampuni yetu itamtumia rasmi Jay-Z kama Mbunifu na Mshauri wetu katika Kampuni. Najua tumeshawahi kufanya hivyo kipindi cha nyuma na Roc Nation, na huu utakuwa ni muendelezo tu“amesema Adam Patrick kwenye mahojiano yake na ESPN.

Wikiendi iliyopita Jay-Z na mkewe Beyonce waliachia album ya pamoja ya ‘Everything is Love’ na tayari wameshaanza tour yao ya OTR II .

 

 

 

Related Articles

Back to top button