Technology

Infinix HOT 30 toleo jipya bei nafuu (+Video)

Samsung na Infinix wanajikuta tena katika ushindani kupitia matoleo haya ‘Infinix HOT 30 na Samsung A14.

Simu zote zimeingia sokoni mwaka huu, Infinix ikiwa ya mwisho kuja sokoni lakini tangu ujio wake Infinix HOT 30 imekuwa ikifanya vizuri ukilinganisha na simu nyengine za daraja la kati kama vile Samsung A14 na nyinginezo.

Hivyo basi, leo tutaangalia features muhimu kama bei, camera, processor, resolution, video features, chajing wat, battery, design, ram na nyinginezo ili msomaji wangu uweze kufanya maamuzi sahihi

‘BOFYA KUONA VIDEO

  • Processor:  Infinix HOT 30 Helio G88 na Samsung A14 Helio G80.

Infinix HOT 30 kwa sasa ndio simu yenye uwezo mkubwa kwenye gaming na yenye kupatikana kwa bei nafuu kulinganisha na simu yengine za daraja la kati.

  • Teknolojia ya fast chaji: Infinix HOT 30 33Wat, A14 15Wat.

Infinix HOT 30 inakuchukua lisaa limoja tu kwa battery ya simu yako kujaa chaji kufikia asilimia 100 lakini Samsung a14 inakuhitaji usubiri kwa masaa mawili kwa battery kufikia asilimia 100.

  • Memory ya ndani: Infinix HOT 30 8GB Ram kuongezeka hadi 16GB Ram/256GB Rom, A14 6GB Ram/128GB Rom.

Ram ya HOT 30 ni kubwa zaidi, Kadri simu yako inavyokuwa na Ram zaidi, ndivyo utendakazi wake unavyoongezeka wakati wa kubadilisha programu. Ikiwa ni mtumiaji wa programu zenye kuchukua nafasi kubwa ya memory kama kuediti video, kucheza games kupitia simu, basi unaweza yafanya haya kwa wepesi kupitia Infinix HOT 30 kwani si rahisi simu yako kugoma goma wala kupata moto. Utendaji kazi wa Ram ya HOT 30 ni hodari mara mbili zaidi kulinganisha na Ram ya Samsung a14.

Eka video landing to Infinix page https://www.instagram.com/p/CrsLQN4ATNA/ 

  • kurecord video: Infinix HOT 30 1440@30fps, A14 1080@30fps.

Kwenye swala zima la kuchukua matukio yaliyo kwenye mwendo au kuchezesha games Infinx HOT 30 ni bora zaidi sababu fremu yake ni kubwa, hivyo hufanya mwendo wa tukio au game uonekane wa asili zaidi na usio na mawimbi ambapo kwa Samsung a14 ipo chini katika technolojia hii na huweza kukufanya usifurahie video ambazo umejaribu kurecord au kudownload na pia kuleta mikwaruzo kwenye kucheza game ya simu.

  • Uang’avu/Resolution: Infinix HOT 30 1080×2460, A14 1080×2408.

Simu zote zinaresolution nzuri isipokuwa ya Infinix HOT 30 imeongezeka uwezo zaidi kama ambavyo inaonekana hapo juu na kadiri resolution inapokuwa kubwa na ndivyo simu yako inavyoweza kuonyesha picha, videos kwa uhalisia na hata uang’avu wa kioo unapozidi kuvutia.

  • Camera kuu ya nyuma kwa simu zote mbili 50MP.
  • Battery zinalingana zote zikiwa na mAh5000.
  • Kioo: Infinix HOT 30 6.78inch, A14 6.6inch.
  • Teknolojia ya kufanya kioo kuwa laini/smooth wakati wa kuperuzi ni 90Hz kwa simu zote.

Sifa nyengine kama kamera, battery, ukubwa wa kioo na refreshrate zinalingana isipokuwa utendakazi wake unaweza pishana, Infinix HOT 30 ni bora kwa sababu ya features kama processor, resolution, video features na fast chaji vinaongeza ubora kwenye kupiga picha kuwa na rangi nzuri na zenye kung’aa, mtumiaji kuokoa muda endapo simu itaishiwa chaji kutokana na fast chaji, refreshrate kufanya kazi kwa wepesi zaidi kutoka na usaidizi wa Ram na processor. 

  • Wembamba: Infinix HOT 30 nyembamba zaidi 8.4mm, A14 9.1mm.
  • Uzito: Infinix HOT 30 haina uzito wa kukera ni gram 196, A14 nzito zaidi gram 201.

Simu zote zinaukubwa wa kioo sawa isipokuwa Infinix HOT 30 ni nyembemba zaidi kitu kinachoifanya ivutie zaidi ukishikia mkononi au kuweka kwenye mfuko wa shati.

  • Bei: Infinix HOT 30 inapatika kwa sh.420,000, inasadikika A14 kuwa sh.450,000.

Kila muuzaji na bei yake isipokuwa InfiniX HOT 30 haizidi kiasi cha sh. 420,000 na Samsung a14 haizidi kiasi cha sh. 450,000.

Kupitia tofauti hizi nadhani nitakuwa nimekusaidia kujua ni simu gani itakupendeza kununua kwa matumizi yako ya kila siku. Lakini pia ubora wa simu sio kuwa na bei kubwa ubora wa simu ni kukupa kile unachokitaka kwa bei yenye kuendana na bidhaa yenyewe.

Ofa

simu zote zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania. Infinix HOT 30 ikiwa na ofa ya GB96 za internet na ofa ya punguzo la bei kwa wanafunzi wa chuo.

Kwa huduma ya haraka wapigie 0745170222 au tembelea @infinixmobiletz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents