Infinix kuwakutanisha washindi wa first 11 star alliance na wakali hawa

Upo tayari ? Kwa mara nyengine tena Infinix inakuletea shindano la “Infinix Star Alliance FIRST 11” na safari hii Infinix imeingia ubia na makampuni mbalimbali kama Boomplay lakini pia inashirikiana na Record lebal ya Msanii maarufu wa kizazi kipya Nahreal, blogger Maarufu Simulizi na Sauti ya Mtangazaji nguli almaarufu Sky pamoja na wanadada kutoka kwenye tasnia ya utangazaji na uimbaji Mimi Mars na Meena Ally kuhakikisha wanakuza vipaji vya washindi 11 wa Infinix FIRST 11 talent search.

Infinix kupitia Shindano hili la Infinix Star Alliance FIRST 11 imedhamiria kuwashika mkono wale wote wenye vipaji na kwa muda mrefu wamejaribu kupambania vipaji vyao lakini bado hawajapata nafasi ya kuonekana. Infinix kuwakutanisha washindi 11 washindano hili la “FIRST 11” kwenye platform stahiki ambazo zitawafanya wasikike.
Kila mshirika atakuwa na kazi kubwa ya kukikuza na kukifanya kijulikana kipaji cha washindi 11 bora wa Infinix FIRST 11.

Tayari imeshafahamika boomplay, record label ya Nahreal na Mimi Mars kukuza vipaji vya washindi wa kuimba kwa kupromote ngoma atayorecordiwa na Nahreal ambayo itakuwa kolabo kati ya mshindi wa FIRST 11 na Mimi Mars na ngoma hii kupromotiwa na Boomplay, Sky na Meena Ally kuhusika na wale wenye vipaji vya kutangaza.

Tangu kuanza kwa shindano hili sasa inapata wiki ya pili na hadi sasa si chini ya watu 413 wamepata kushiriki #infinixfirst11.

Chakufanya jiricord sasa ukiwa unaonyesha talent yako yoyote kama kuimba, kucheza, kutangaza, kuchora, kuimba na kadhalika kisha post katika Instagram account yako na #infinixfirst11 ushindi wako pia unategemeana na mashabiki watakavyoshiriki katika kuipatia likes post yako.

Ikumbukwe Star Alliance ilianza rasmi mwanzoni mwa mwezi wa 4 kampuni hii ya simu ikiwa mbioni kuzindua Infinix NOTE 10 simu pendwa kutokana na ubora wa camera yenye MP64 na design ya kuvutia.

Katika shindano hilo washindi 10 wa kwanza waliondoka na Infinix NOTE 10 na vitita vya pesa ambapo mshindi wa kwanza aliondoka na takribani sh.Million 5, wapili sh. Million 2,500,000 na mshindi wa tatu hadi wa kumi walijizolea kitita cha sh. 1,150,000 kila mmoja.

Infinix imekuwa moja ya kampuni yenye kuonyesha support kubwa sana kwa vijana tangu kuingia kwake nchini Tanzania Infinix imekuwa ikijikutanisha na vijana kupitia mbinu mbalimbali kama uandaaji Midahalo, Challenge search lakini pia udhamini wa vipindi mbalimbali vya vijana kama kipindi cha Bongo Star search n.k.

Zawadi nyengine ambazo zitatolewa katika shindano hili la Infinix FIRST 11 ni simu aina ya NOTE 11 ambayo bado kuingia sokoni rasmi na hizi ni baadhi ya sifa zake AMOLED screen 6.7 FHD+, 5000mAh na 5000Wh.

Tembelea @infinixmobiletz kupata habari za haraka kuhusu challenge hii ya Infinix FIRST 11.

Related Articles

Back to top button