HabariTechnology

Infinix kuzindua mfumo wa kuchaji simu kupitia Nishati ya Mwanga

Ushawahi kuwa na ndoto ya siku moja utumie mwanga wa jua kuchaji simu janja yako?!. Kama jibu ni “ndio” basi unapaswa kufahamu kwamba Ndoto hiyo inakwenda kutimizwa na Infinix siku chache zijazo ambapo wanakwenda kutambulisha mfumo wa kuchaji simu kwa kutumia nishati ya Jua/Mwanga ndani ya ShowStoppers MWC 2025.

 

Infinix inaendelea kusimamia misingi yake ya kuboresha maisha ya watumiaji wa simu janja na Mwaka huu kupitia ShowStoppers MWC, wamepanga kutambulisha mfumo huu mpya wa kimageuzi utaoanza kupatikana katika matoleo yao ya jayo ya Simu wakiwa na lengo la kuunga mkono harakati za utunzaji wa mazingira kupitia matumizi ya nishati salama na kuachana na matumizi ya nishati haribifu ya mazingira.

Nje ya utunzaji wa Mazingira mfumo huu pia utakwenda kubadilisha kabisa maisha ya watumiaji wa simu janja kwani utakuwa na moenekano wa kisasa na saidizi zaidi kwa watumiaji wao haswa wanaopatikana katika maeneo yasiyo na upatikanaji wa Umeme.

Mfumo huu unakuja na :

Uwezo wa kuhifadhi chaji kwa muda mrefu na kuweza kujichaji wenyewe (automatic) kupitia mwanga wa Taa za ndani na nje hata kama kukiwa na wingu zito.

Uwezo wa kumuweka hewani mtumiaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kuweza kuchajisha popote pale na wakati wowote.

Inahusisha AI yenye MPPT (Maximum Power Point Tracking) inayoipa uwezo wa kudhibiti voltage na kupunguza uongezekaji hovyo wa joto la betrii pindi inapokuwa katika mazingira magumu ama kazi nzito.

Bado haijawekwa wazi ni Toleo gani hasa la Infinix litakuwa lakwanza kuwa na aina hii mpya ya teknolojia hivyo ni utambulisho tu wa namna Kampuni hii inawaza kwa niaba ya binadamu wote namna bora ya kuboresha matumizi ya Simu Janja katika hali ya utunzaji wa mazingira kwa miaka ijayo.

Kwa mawasiliano zaidi tembelea kurasa zetu za kijamii @infinixmobileTz au piga simu +255760552543

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents