Infinix wamaliza kila kitu, Simu mpya na maajabu yake – (Video)
Siku ya Jana Kampuni ya Simu ya Infinix Mobile TzĀ imezindua simu mpya aina ya Infinix Note 40 ambayo imekuja na mabadiliko makubwa sana.
Akiongea na wana habari Afisa Mahusiano wa Infinix Mobile Tz Aisha, ameeleza kwa urefu ubora wa simu yao mpya ya INFINIX NOTE 40.
Simu hii imekuja na vitu vingi vya kuvutia ikiwemo Fast Charger ambayo ni Wireless ikitumia dakika 15 kujaa na unaweza kuchajisha simu mbili kwa wakati mmoja.
Mbali na kuwa na uwezo mkubwa na Camera kuwa unaweza kuchukua matukio mawili kwa wakati mmoja pia storage ya ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 12.
Kubwa zaidi ukinunua unapewa bando la GB 96 kwa mwaka na pia Tiketi ya AIR Tanzania kwenda Dubai na China na pia baadhi ya maeneo hapa Tanzania ambayo utaweza kuitumia muda wowote ndani ya mwaka mzima endapo utashinda Droo maalumu watakayoianzisha.
Badfo unataka nini tena zaidi ya kununua INFINIX NOTE 40 na INFINIX NOTE 40 PRO.
Vido kamili angalia youtube ya Bongofive: