Inter Milan mabingwa wa Serie A baada ya miaka 10

Klabu ya Inter Milan kwa mara ya kwanza yatwaa Ubingwa wa Serie A baada ya miaka 10 kupita, hii ni mara baada ya Sassuolo kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Atalanta na kuwa hakikishia vijana wa Antonio Conte kulitwaa rasmi taji hilo.

Inter inatangaza ubingwa ikiwa mbele kwa pointi 13 dhidi ya yule anaemfuata kwenye msimamo wa ligi huku akiwa bado amesaliwa na michezo minne mkononi na kuvunjiliambali utawala wa Juventus.

Juventus imekuwa ikilichukua kombe hilo kwa miaka nane mfululizo bila kuliachia hatimaye msimu huu Inter Millan imevunja mwiko.

Mara ya mwisho Inter Milan kuchukua Ubingwa ilikuwa mwaka 2010.

Related Articles

Back to top button