Irene Uwoya na Steve Nyerere waitwa BASATA, ‘Kile kitendo kimetuudhi, Tutahitaji maelezo zaidi’

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaita waigizaji wawili wa filamu, Irene Uwoya na Steve Nyerere kufika katika ofisi za Baraza hilo, Kesho Julai 17, 2019 kufuatia tukio la kuwarushia fedha Waandishi wa Habari kwenye kikao chao kilichofanyika jana Julai 15.

Akithibisha taarifa hiyo kwenye mahojiano yake na Bongo5, Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa wamewaita wasanii hao ili kuongea nao kuhusu tukio hilo.

Ndio tumewaita, Kikubwa zaidi tutataka kuongea nao kuhusu lile tukio. Sisi kama walezi wa sanaa hatujalipokea vizuri, tutahitaji maelezo zaidi. Mengine tutaongea zaidi hiyo kesho,“amesema Mngereza.

Hata hivyo, tayari Irene Uwoya amewaomba radhi waandishi wa habari, kufuatia kitendo hicho kilichopelekea baadhi ya waandishi kuharibu vifaa vyao vya kazi.

Irene amesema hakufanya hivyo kwa lengo la kudhalilisha waandishi wa habari kama watu wengi wanavyotafsiri bali alifanya kama kuwatunza waandishi kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Related Articles

Back to top button