FahamuHabariSiasa

Israel imeruhusu njia moja raia wa Gaza kupita kabla ya mashambulizi

Maelfu ya Wapalestina wanaendelea kutoroka kaskazini mwa Gaza kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa ya Israel.

Njia ya kuwahamisha watu wa Gaza wanaotoroka kaskazini mwa eneo hilo imefunguliwa muda mfupi uliopita.

Israel inasema raia wanapaswa kusafiri kwa njia kati ya 10:00 na 13:00 saa za ndani (07:00 na 10:00 GMT).

Wanapaswa kutumia njia moja inayotoka Beit Hanoun kuelekea Khan Yunis, linasema, na kuongeza kuwa haitalenga njia wakati wa saa hizo.

IDF imebadilisha saa za uhamishaji katika siku chache zilizopita.

Tarehe ya mwisho ya kuhama ya awali ya saa 24 iliyotangazwa Ijumaa, ilipita Jumamosi alasiri.

Wakati huo, Israeli iliteua njia mbili – moja wapo ilikuwa njia ile ile ambayo IDF imetaja leo.

Shirika la Afya Ulimwenguni limelaani agizo la kuhamishwa, na linasema kuwalazimisha wagonjwa hospitalini kuhama itakuwa “hukumu ya kifo”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents