Israel inasema jumba la habari walilolilipua lilitumiwa kuwaharibia mipango (+ Video)

Israel inasema jumba la habari lililolipuliwa na moja ya makombora yake ya angani katika mzozo wa Gaza wa hivi karibuni lilikuwa likitumiwa na kundi la wanamgambo wa Hamas kujaribu kuharibu mfumo wake wa kujikinga dhidi ya makombora.

Jumba la Jala lilikuwa na ofisi za shirika la habari la Associated Press (AP) na Al Jazeera.

Akielezea AP juu ya shambulio hilo mjini New York, mjumbe wa Israel katika Umoja wa Mataifa pia alijitolea kusaidia ujenzi wa ofisi zake mjini Gaza.

AP ilikaribisha mkutano huo lakini inasema haijapata ushahidi wa kuthibitisha madai ya Israel.

Hamas, kundi la wanamgambo wa Kipalestina ambalo linaoongoza Gaza, halijatoa tamko lolote kuhusu madai ya Israel.

Mzozo wa hivi karibuni ulianza baada ya wiki kadhaa za mvutano kati ya Israeli na Wapalestina kuhusu makazi ya Jerusalem Mashariki kuishia kuwa mapigano katika mji huo mtakatifu unaogombaniwa na Waislamu na Wayahudi.

Hamas walianza kurusha maroketi nchini Israel baada ya kuitaka nchi hiyo kuondoka katika eneo hilo, nao Israel wakalipiza kisasi kwa mashambulio ya angani katika ngome zao mjini Gaza.

Siku kumi na moja za makabiliano makali zilisababisha vifo vya watu 256 huko Gaza, kulingana na Umoja wa Mataifa (UN), na watu 13 waliuawa nchini Israeli, kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa mnamo Mei 21.

UN ilisema karibu watu 128 waliouawa Gaza walikuwa raia. Majeshi ya Israel yalisema watu 200 kati yao walikuwa wanamgambo; Kiongozi wa Hamas mjini Gaza,Yahya Sinwar, anasema ni wapiganaji 80 waliuawa.

Toeni ushahidi kamili

Kufuatia shambulio dhidi ya jumba hilo mnamo Mei 15, AP na Al Jazeera ziliomba maelezo kutoka kwa serikali ya Israel.

Mjumbe wa Israel katika Umoja wa Mataifa na balozi wa Marekani, Gilad Erdan, alitembelea ofisi za AP mjini New York siku ya Jumatatu nayo majeshi ya ulinzi ya Israel yakatoa taarifa siku ya Jumanne.

Bw. Erdan amewaambia viongozi wa ngazi ya juu wa shirika hilo la habari la Marekani kwamba jumba hilo lililokuwa na ofisi zake mjini Gaza l ilikuwa linatumiwa kuendesha shughuli za kuvuruga mitambo yake ya kujikinga dhidi ya makobora.

 

Alisema Israel haikuwashuku wafanyakazi wa AP “walikuwa na taarifa kwamba Hamas wanatumia jumba hilo kufanya oparesheni zake”.

Bwana Erdan alisema Israel “inazingatia umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari,” akiongeza: “Israel inajitolea kuisaidia AP kujenga tena ofisi zake na shughuli zake mjini Gaza.”

Destroyed tower in Gaza

Taarifa za Jeshi la Ulinzi la Israel ilisema Hamas ilikuwa ikitumia jumba hilo kufanya intelijensia ya kunasa mawasiliano ya oparesheni yao ya kielektroniki.

Zaidi ya maroketi 3,000 yalirushwa nchini Israel kutoka Gaza wakati wa mzozo na majeshi ya Ulinzi ya Israel yanasema mtambo wa kujikinga dhidi ya makombora ulidungua asilimia 90 ya makombora hayo.

Bofya hapa chini kutazama jinsi lilivyolipuliwa.

https://www.instagram.com/tv/CP5e2h9h-Ak/

Related Articles

Back to top button