
Msanii wa muziki kutoka kiwanda cha Bongo Fleva @jaivah anazidi kuchimbia mizizi katika Taifa la Nigeria kwenye upande wa Burudani.
Baada ya wimbo wake wa KAUTAKA kumfungulia milango Nigeria watu walihisi labda hataweza kufanya kazi zingine zitakazopenya Nigeria.
Jamaa ameendelea kufanya Vizuri Nigeria kupitia ngoma zake zingine na yeye ameamua kuwekeza muda wake kwenye Taifa lile ambalo ndio linaongoza kwa biashara ya muziki Afrika.
Kwenye hii video anatumbuiza ngoma yake ya NAOGOPA MAPENZI
Valentine ya mwaka 2025 @jaivah kakiwasha tena Nigeria na inaelezwa sio tu Valentine mpaka sasa bado anaendelea kupiga Show kule.
Hapa ni katika Jiji la Benin Edo State lililopo Nigeria na mwamba amekiwasha kama kawaida yake.
Neno moja kwa @jaivah
Credit by @el_mando_tz