Habari

Jaji Mkuu awataka watu wasioridhishwa na maamuzi ya mahakama kukata rufaa

Jaji Mkuu wa Tanzania,  Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa rai kwa watu wasioridhishwa na maamuzi yanayotolewa katika mahakama kukata rufaa kwa kuwa ni haki yao.

Aidha Jaji Juma amewataka pia Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Majaji wote nchini kutoa haki kwa kuzingatia mizani ya haki bila kuyumbishwa na mitazamo inayotolewa na watu baada ya hukumu kusomwa.

Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo mkoani Arusha.

Prof. Juma ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania unaofanyika kwa siku tatu mkoani hapa.

Hata hivyo majaji hao wamekutana mkoani Arusha kwa lengo la kukumbushana na kubadilishana uzoefu kuhusu majukumu ya Majaji hao na nafasi zao katika maboresho ya Mahakama na kupitia maboresho ya Mhimili huo ili kufanikisha ustawi wa wananchi kwa ujumla.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents