Habari

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuzungumza na M23 – Angola

Ofisi ya rais wa Angola imetangaza kuwa itawasiliana na vuguvugu la M23 ili kundi la DRC na M23 “wafanye mazungumzo ya moja kwa moja”.

Tina Salama, msemaji wa Rais Tshisekedi, hakuwa na uhakika kuhusu tangazo la Angola, lakini aliiambia tovuti ya X kwamba Angola “itachukua hatua zinazohusiana na upatanisho”.

“Tunasubiri kuona utekelezaji wa mchakato huu wa upatanishi wa Angola,” Tina aliongeza.

Hii ilitangazwa baada ya ziara “fupi” ya Rais Félix Tshisekedi wa DR Congo huko Luanda ambako alikutana “peke yake” na mwenzake João Lourenço wa Angola.

Rais Lourenço, ambaye amekuwa mpatanishi katika mzozo wa DR Congo kwa karibu miaka minne, alitangaza mwezi uliopita kwamba atajiuzulu kutoka kwa majukumu hayo ili kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambayo ingethibitishwa.

Serikali ya DRC imekuwa ikikataa wito wa mazungumzo ya kikanda yaliyoitishwa na SAD, na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wa kufanya mazungumzo na waasi wa M23, jambo ambalo lilikwamisha utekelezwaji wa maazimio ya vikao vya Luanda, Dar es Salaam na Nairobi.

Rais Tshisekedi alisema wazi kwamba “maadamu mimi ni rais wa DR Congo” kamwe hatajadiliana na M23, kwamba mazungumzo na kundi hili analoliita la kigaidi ni “mstari mwekundu ambao hatutavuka kamwe”.

Hatua ya Rais wa DRC kukubali kufanya mazungumzo na M23, inaonelewa kama hatua muhimu katika juhudi za kurejea kwa amani katika eneo la maziwa makuu

Wakati haya yakijiri SADC inatarajia kuitisha mkutano utakaojumuisha serikali ya DRC na wasi wa M23 kutafuta suluhu ya amani.

Serikali ya DRC pia imelaumiwa na Rwanda kwa kutotekeleza mazungumzo ya Luanda kuhusu kuwaondoa wapiganaji wanaopigana dhidi ya serikali ya Rwanda wa kundi la FDLR wanaoendesha harakati zao DRC.

Kwa upande wake DRC imekuwa ikiituhumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23 , shutuma ambayo Rwanda imekuwa ikizikanusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents