Habari

Jaribio la mapinduzi lazimwa Sudan

Kituo cha Tevisheni cha taifa nchini Sudan kimeripoti asubuhi ya leo kwamba kumefanyika jaribio la mapinduzi ambalo limeshindwa. Msemaji wa serikali kupitia kituo cha Televisheni cha taifa amesema viongozi wa jaribio hilo la mapinduzi wamekamatwa.

Duru za maafisa waaandamizi wa kijeshi na serikali nchini Sudan zimeliarifu shirika la habari la AFP kwamba jaribio hilo limehusisha kundi la maafisa ambao wametimuliwa mara moja baada ya juhudi zao za kutaka kulidhibiti jengo la shirika la utangazaji la taifa.

Taher Abuhaja afisa wa ngazi ya juu katika baraza la uongozi la nchi hiyo amesema jaribio la kutaka kuchukua madaraka limezimwa. Aidha Afisa mwingine mwandamizi katika baraza hilo, Mohamed al Fekki nae ameeleza kwamba kila kitu kimedhibitiwa na utawala wa kimapinduzi uko imara.

Vikosi vya usalama inaarifiwa kwamba vimelifunga daraja kuu la kupita Mto Nile linalouunganisha mji wa Khartoum kwenda mji wa Omdurman. Sudan inaongozwa na serikali ya mpito iliyopatikana baada ya kuondolewa kwa nguvu madarakani rais wa zamani Omar al Bashir, serikali ambayo inawajumuisha wajumbe wa kijeshi na kiraia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents