Jay Moe aeleza kwanini hakukata tamaa licha ya kuwa msanii mwenye ‘gundu’ kwa miaka mingi

Rapper Jay Moe Moe amesema yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakisemwa wana gundu na hawana bahati.

Lakini hilo halikumkatisha tamaa na kuzidi kusonga mbele katika fani yake ya kurap ambayo sasa anayaona mafanikio yake baada ya miaka 17 kwenye game.

Jay Moe ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na mtangazaji Bob danta kwenye kipindi cha Weekend Night cha TBC Taifa, na kuzidi kuwapa moyo wasanii ambao bado hawajapata mafanikio katika kile wanachokiamini, kutokata tamaa na kuzidi kufanya vizuri zaidi kwenye muziki ambao wanaufanya.

Jay Moe kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake Nisaidie Kushare, amezidi kufanya vizuri kwenye game ya hip hop tangu aliporudi na kibao chake cha Pesa ya Madafu.
Mtazame zaidi hapo juu.

Related Articles

Back to top button