Burudani

Jay Z haniwezi kabisa – Ludacris

Mwigizaji na Mwanamuziki kutoka Marekani Ludacris amedai kuwa msanii Jay Z hamuwezi katika Uandishi wa mistari ya nyimbo na endapo wangepewa masaa mawili ya kuandika basi yeye angeibuka kuwa mshindi.

Ludacris ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye Podcast ya (Funky Friday) ambapo ameeleza kuwa japo siku za hivi karibuni kumekuwa na ushindani mkubwa katika muziki wa Hip-Hop lakini anaamini kuwa Jay Z hamuwezi patika uandishi wa Verse.

Ikumbukwe kuwa Ludacris aliwahi kumshirikisha Jay Z katika wimbo uitwao “I Do it for Hip Hop” uliyopo kwenye album yake ya mwaka 2008 ya “Theatre of the Mind”.

Mkali huyo ambaye ameonekana katika filamu ya “Fast and Furious” amekuwa akitamba na ngoma zikiwemo “Act a Fool”, “What’s Your Fantasy”, “Get Back” huku akionekana katika filamu kama “Dashing Through the Snow”, “Crash”, “Hustle & Flow na nyinginezo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents