Burudani

Je, kweli Vera Sidika ni mjamzito?, mpenzi wake ‘Otile Brown’ ajibu

Penzi la video vixen maarufu nchini Kenya, Vera Sidika na mpenzi wake Otile Brown ambaye ni mwanamuziki bado linagonga vichwa vya habari.

Time hii ni Otile Brown kafunguka kuhusu mipango ya kufunga ndoa na Vera Sidaka na iwapo mrembo huyo ni mjamzito.

Muimbaji huyo katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm alipoulizwa kuhusu Vera kuwa mjamzito, alijibu; ‘Hilo sita-comment kwa sasa’.

Hata hivyo suala la kufunga amelizungumzia kwa kueleza kuwa chochote kinaweza kutokea.

“Yeah, why not, she is smart, she is intelligence, mwanamke mwenye hekima halafu ni mpambanaji, so i just love everything about her, chochote kinaweza kutokea,” alisema Otile Brown.

Mwanzoni mwa May, 2018 kulisambaa taarifa na picha kuwa Vera Sidika ana ujauzito wa Otile Brown, hata hivyo baadae ilikuja kubainika kuwa ujauzito huo ulikuwa bandia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents