Technology

Je, tunahitaji uzoefu wa Kazi ili kuweza kuajiriwa?

Imekuwaikiwapawakatimgumusanahasa wale wanaokuwa wamemaliza masomo yao kwa muda mfupi na kuingia katika harakati za kutafuta ajira.  Ofisi nyingi sana hasa Mashirika Binafsi (yasiyo ya Kiserikali) na Makampuni binafsi yamekuwa yakiongeza suala la Uzoefu wa kazi kama kigezo cha kupata ajira. Hivyo kampuni ya simu ya Infinix ikaona ni vyema kuwakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo kuweza kujadili suala hili kupitia mdahalo unaosema “Je, tunahitajiuzoefu wa kaziilikuwezakuajiriwa?” ambapo ili fanyika katika Ukumbi wa Sahara Ventures uliopo Morocco siku ya Jumamosi Tarehe 10/04/2021.

Mdahalo huu uliwataka vijana kujigawa katika vikundi viwili wenye kukubaliana na mada ambao walifahamika kama Kundi Black na kundi White wenye kupinga kwamba ili kuajiriwa uzoefu si kitu cha lazima.

Mdahalo huu uliongozwa na watu Maarufu kama vile MC. Anthony Luvanda, Bi. Shamila Mshangama na Mr. Erick Benard (Mr. Ben)

Mchuano ulikuwa ni mkali mno kuanzia kwenye vikundi hivyo viwili hadi kwa wageni waalikwa ambao ndio walikuwa kama majudge na waongozaji wa mdahalo mzima.

Bi. Shamila alianza kwa kuipinga mada “kupata kazi sio lazima uwe umeajiriwa maana unaweza kujiajiri kwa kuwa na taasisi ambapo unaweza kuonwa kutokana na juhudi ulizo fanya, hivyo utakuwa umepata uzoefu kupitia hapo lakini huja ajiriwa”.

Lakini pia MC Luvanda aliikataa hoja kwa kusema “unaweza kuwa huna uzoefu wowote na bado ukafanya vizuri saana na mwenye uzoefu asifanye vizuri pia”.

Vijana wote katika makundi yao nao walionekana kuwa wamejiandaa vyakutosha kila upande ukiwa na hoja zenye kujitosheleza iliyopelekea kutopata mshindi mmoja kwani kila mmoja aliibuka kidedea na kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile Simu, Tshirt, Wireless Keyboards za kompyuta pamoja na Note 8 package iliyokuwa na vitu mbalimbali kama (Mwamvuli, Notebook, Power bank, chupaya chai/maji, zilizo andaliwa na Mdhamini Mkuu ambayo ni kampuni yenye kuji husisha na uzalishaji wa simu janja Infinix Mobile.

Infinix Pamoja yakuwa ni kampuni iliyojikita kwenye soko la simu lakini pia ni kampuni yenye kumjali Zaidi mwanafunzi wa leo kwa kumuandaa kwajili ya kesho yake. Kupitia XTOK Infinix imeweza kuwafikia wanafunzi wengi sana kwa wakati mmoja ambapo kila mwanafunzi hujifunza kitu kipya katika Tafrija hii ya XTOK.

 

Infinix mobileTz kuwaahidi vijana na wote waliohudhuria kwenye mdahalo huu kuwa wataku wanao Pamoja kwenye shughuli zote za vijana na pia kuwasihi wasikose mdahalo ujao kwakuwapa nafasi pia wao kuchagua mada ambayo itakuwa ya Xtok inayofata, mada inaendelea kwenye kurasa zao za kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter na pia kwenye kiunga chao cha Xclub.

Tembelea link hiikuonamdahalohuuulivyoendahttps://www.instagram.com/p/CNmyuLYHfO_/?igshid=o67ietlqew7k

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents