Habari
Je, unajua kwanini pamoja na hasara ya mashirika ya Umma lakini hayafungwi, Mr Kafulila afunguka makubwa
Mkurugenzi wa PPP – Centre Mr David Kafulila amefunguka juu ya Tanzania kutambuliwa Kimataifa kama mlango mkuu wa Uchumi Afrika, hii inatokana na sababu ya Nchi ya Tanzania kuzungukwa zaidi na mataifa ambayo hayapo upande wa bahari kwahiyo hawana budi kutumia Bandari ya Tanzania.

Ikumbukwe tu Bahari ni njia kubwa zaidi inayotumika katika masuala ya ukuaji wa Uchumi Duniani, Pia amegusia watu wengi kutokuelewa jinsi ya tafsiri ya baadhi ya mashirika baadhi ya Serikali kupata hasara kuwa kuna aina mbili za hasara lakini serikali inaangalia zaidi faida ya kiuchumi kwa maana hiyo hasara za kihasibu zinazibwa na faida ya kiuchumi inayopatikana nchini na kutolea mfano shirika la Ndege la Tanzania ndio maana haliwezi kufungwa.




