BurudaniHabari

Jeff Bezos auvalisha pete mchepuko uliyevunja ndoa yake

Mchepuko uliopelekea ndoa ya Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos (59) kuvunjika mwanadada ambaye pia ni Mwandishi wa Habari Lauren Wendy Sánchez (53) hatimaye mchepuko huo umekuwa rasmi mchumba wa Jeff Bezos.

Ikumbukwe kuwa Mnamo mwaka 2019 bilionea huyo alimpa talaka aliyekuwa mke wake MacKenzie Scott  baada ya kusambaa habari kuwa wameshindwa kuendelea na ndoa yao baada ya mke wake kugundua kuwa mume wake Jeff yupo kwenye mahusiano na mwandishi huyo wa habari.

Sakata hilo lilipelekea ndoa hiyo kuvunjika lakini pia kwa upande wa mwanadada Lauren Wendy Sánchez  naye ndoa yake ilivunjika baada ya mume wake kusikia kuwa Jeff Bezos amevunja ndoa yake kisa yuypo kwenye mahusiano na Mke wake, naye akaona alaaah haiwezekani kabiusa naye akamuacha mke wake ambaye ndio amevalishwa pete na Jeff.

Sasa taarifa zinasema kuwa mchepuko huo umevisha pete ya uchumba ndani ya yacht ya bwana Jeff Bezs yenye thamani ya dola Milioni 500. sawa na zaidi ya Trilioni moja za KitanzaniaKwa mujibu wa vyombo vya habari na watu wao wa karibu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents