HabariMichezo

Jengo la Yanga lanusurika Kubomolewa

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema jengo la Timu ya Yanga si sehemu ya nyumba zitakazobomolewa katika mradi wa bonde la Mto Msimbazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa nyumba zitakazobomolewa tayari wahusika walifahamishwa na wengine wamekwisha lipwa fidia amewaondoa shaka mashabiki wa Yanga kuwa jengo la timu yao halipo kwenye orodha hiyo.

‘Kufikia Februari 29, 2024 TARURA ililipa fidia Tsh Bilioni 52.6 kwenye akaunti za wamiliki wa nyumba wapatao 2,155 kati ya 2,329 ambao walikuwa wameandikishwa kwenye daftari la kwanza, hivi sasa TARURA inakamilisha malipo ya fidia kwa wahusika wengine 446 waliomo kwenye daftari la pili amesema Matinyi.

Ameongeza kuwa shughuli za kubomoa nyumba hizo itaanza April 15 mwaka huu na inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu hadi kukamilika kwake.

Mradi wa bonde la Mto Msimbazi unatarajiwa kugharimu Sh bilioni 675 na utakamilika ndani ya miaka mitano.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents