Burudani

Jennifer Lopez achumbiwa tena na Ben Affleck

Mugizaji na muimbaji Jennifer Lopez ametangaza kuwa atafunga pingu za maisha na Ben Affleck, miaka 18 baada ya wapenzi hao kusitisha harusi yao.

Lopez, 52, alidokeza kuwa amechumbiwa kwa mara ya pili na nyota wa Hollywood Affleck katika ujumbe aliyoweka katika mtandao wake wa OnTheJLo.

Alitania jinsi alivyokuwa na “tangazo kuu” katika chapisho kwa wafuasi wake milioni 202 wa Instagram siku ya Jumamosi.

Lopez hata hivyo alisema wale ambao si “wandani wake wa karibu” watalazimika kujiunga na tovuti yake, ambapo anashirikisha “masuala zaidi ya kibinafsi”, ili kujifunza habari zake, aliongeza.

JLO anaonekana akilia kwenye video huku akivutiwa na pete kubwa ya kijani ya uchumba.

Uvumi kwamba wawili hao wamerudiana tena ulizuka baada ya kupigwa picha ya pamoja mwezi Mei mwaka jana.

Lopez alithibitisha rasmi kwamba wamerudiana kupitia chapisho la Instagram akimmbusu mpenzi wake kwenye yacht huko St Tropez,siku yake ya kuzaliwa ya 52.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents