Habari

Jeshi la polisi lathibitisha kumkamata mwandishi Erick Kabendera, ni baada ya kukataa wito wa kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Mwandishi wa habari, Erick Kabendera mwenye umri wa miaka (39) mkazi wa Mbweni kwa kutotii wito wa Jeshi la Polisi.

Image

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi imesema kuwa mwandishi huyo aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano na kukaidi.

”Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia ERICK KABENDERA, (39) mkazi wa Mbweni, Mwandishi wa habari, kwa mahojiano. Mnamo tarehe 29/07/2019 mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake na Jeshi la Polisi baada ya kukataa wito wa Jeshi la Polisi,” – Taarifa iliyoandikwa na Jeshi la Polisi.

Jeshi hilo la kanda maalum Dar es Salaam limeongeza ”Aidha mwandishi huyo awali aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi wito huo. Ndugu waandishi wa habari niseme utii wa sheria bila shuruti ni muhimu sana kuzingatiwa kwani ukishindwa kutii sheria inakuwa shuruti.”

”Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali zikisambaa kuwa mwandishi huyo ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hajatekwa ila tumemkamata kwa mahojiano. Aidha mtuhumiwa huyo kuna mashaka makubwa kuhusiana na uraia wake tutakapobaini mara moja tutamkabidhi kwenye idaya ya uhamiaji ili kushughulika naye na ndiyo maana alikuwa akikaidi wito wa polisi na kujihami kuwa ametekwa.”

Kwa upande mwingine Jeshi hilo limetoa taarifa ya kumshikilia Daudi Ranadhani Iddy mwenye umri wa miaka (23) mkazi wa Tabata kwa kosa la kujifanya Polisi na kuvalia sare zenye cheo cha mkaguzi msaidizi.

”Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linamshikilia DAUDI RAMADHANI IDDY (23) mkazi wa Tabata Segerea kwa kujifanya ofisa wa Polisi, akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na cheo cha mkaguzi msaidizi wa Polisi( Assistant Inspector).”

”Mnamo tarehe 19.07.2019 Jeshi la Polisi lilipata tarifa toka kwa askari wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) makao makuu Mlalakuwa, kuwa kuna kijana mmoja amevaa sare za Jeshi la Polisi wana mashaka naye.”

”Makachero wa Jeshi la Polisi walifika makao makuu ya JKT Kumkamata na kufanya naye mahojiano,mtuhumiwa alikiri kujifanya yeye ni afisa wa Polisi na kufanya utapeli.”

Pia alikiri kupitia mafunzo Jkt huko Mafinga mwaka 2006 na kujitolea kwa mujibu wa sheria katika kambi hiyo. Mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi na kupatikana na vifaa vifuatavyo;

”1.sare moja ya Polisi aina ya kaki 2. vyeo vya(Cpl, Sgt na cheo cha mkaguzi msaidizi 3 pea moja inaya kombati Jungle green. 4.pingu moja. 5.kofia moja ya askari wa usalama barabarani. 6.radio ya upepo moja aina ya motorola.7 mikanda miwili ya Jkt.8.mkanda mmoja wa bendera wa Jeshi la Polisi, buti na viatu vya kawaida. Upelelezi wa kina unaendelea na mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents