Habari

Jeshi lakubali kumrejesha Waziri Mkuu madarakani, Sudan

Maafisa wa kijeshi na serikali nchini Sudan wamesema leo kuwa makubaliano yameafikiwa kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia kumrejesha madarakani Waziri Mkuu aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya Oktoba 25 Abdalla Hamdok.

Hamdok: Man of the moment on Sudan's future - The East African

Viongozi hao wameongeza kuwa maafisa wa serikali na wanasiasa waliokamatwa tangu mapinduzi hayo wataachiwa huru kama sehemu ya makubaliano hayo kati ya jeshi na vyama vya kisiasa, ikiwa ni pamoja na Chama kikubwa cha Umma.

Maafisa hao wameongeza kuwa Hamdok ataongoza baraza huru la kitalaamu la mawaziri na kwamba Umoja wa Mataifa, Marekani na wadau wengine walitekeleza jukumu muhimu katika kuafikia makubaliano hayo.

Maafisa hao waliozungumza kwa sharti la kutotambulishwa kwa kuzungumzia makubaliano hayo kabla ya kutangazwa rasmi, wamesema kuwa baraza hilo kuu jipya litakutana baadaye leo kabla ya kutoa tangazo lake. Mohmmed Youssef al-Mustafa, msemaji wa chama cha wataalamu wa Sudan SPA, amesema makubaliano yameafikiwa lakini chama hivo kitatoa maoni yake tangazo hilo litakapotolewa rasmi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents