Habari

JKCI, wataalamu wa afya kutoka Misri kuwatibu wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imewaomba wataalam wa afya kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya kuziba kwa mishipa ya damu ili watibiwe katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya kuzibua mishipa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na JKCI imeeleza kuwa matibabu hayo yatatolewa Septemba 22 hadi 28, 2024 yatafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya Andalusia ya nchini Misri.

Imeelezwa matibabu yatakayotolewa katika kambi hiyo ni ya kuzibua mishipa ya damu ya artery iliyoziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab, upasuaji kwa njia ya kutumia matundu madogo katika kutibu mishipa ya damu ya vein iliyotanuka kwa kutumia kifaa cha umeme kijulikanacho kwa jina la laser ablation.

Matibabu mengine yatakayotolewa ni kuzibua mishipa ya damu (veins) ya shingo iliyoziba (ballooning) kwa kutumia mtambo wa Cathlab hasa kwa wagonjwa wa dialysis wanaotumia catheter kwaajili dialysis.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa inawaomba wagonjwa wenye matatizo ya ganzi miguuni, vidonda vya miguu visivyopona kwa muda mrefu, matatizo ya mishipa ya damu miguuni

written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents