Michezo
John Bocco kuwa mchezaji anayelipwa zaidi

Nahodha wa zamani wa Azam na Simba John Raphael Boko amevuta zaidi ya Tsh. 50 milioni kutoka JKT Tanzania ikiwa ni fedha kwa ajili ya usajili ‘signing fee’.

Boko atakuwa akilipwa mshahara wa Tsh. 6 milioni kwa mwezi kwa kipindi chote cha mkataba wake na yeye ndio mchezaji anakunja kiasi kikubwa cha mshahara kwa wachezaji wote wa JKT Tanzania.




