Michezo

Jose Mourinho aitabiria mema Uingereza dhidi Tunisia leo kombe la dunia

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anaamini kuwa timu ya taifa ya Uingereza itaibuka na ushindi dhidi ya Tunisia hii leo michuano ya kombe la dunia inayo endelea nchini Urusi.

Ukilinganisha na vigogo wengine kupoteza kama Ujerumani na wengine kutoka sare kwenye michezo yao ya ufunguzi ya michuano hiyo mikubwa na inayofatuatiliwa na wengi, Mourinho anaamini kuwa Uingereza watafanikiwa kuibuka na alama tatu kwenye mechi hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa hapo baadae jioni leo siku ya Jumatatu.

Mourinho ameiyambia Russia Today kuwa “Nilitazama mchezo wa kirafiki wa Tunisia dhidi ya Ureno kabla ya michuano hii ya kombe la dunia kuanza na ukweli sikupendezwa nayo,” amesema Mourinho.

Kocha huyo wa Man United ameongeza “Nailinganisha Tunisia na timu ya taifa ya Morocco kwa aina ya uchezaji wake na kikosi chake kilivyo hivyo nadhani Uingereza itaweza kushinda mchezo huu”. Hata hivyo Brazil ilipaswa kushinda, Ujerumani na hata Argentina lakini sijajua kwa nini wameshindwa kufanya hivyo.”

“Leo ni siku ambayo timu imara na yenye vikosi madhubuti ambazo ni Uingereza na Ubelgiji watashuka dimbani kucheza kwahiyo wacha tuone timu changa zitajifunza nini kutoka kwao.”

Timu za taifa za Hispania, Argentina, Ujerumani na Brazil zimeshindwa kufanya vizuri kwenye michezo yao ya kwanza ya ufunguzi kwenye michuano hii ya kombe la dunia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents