Michezo

Joto la Dar limetufanya tufungwe – Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane (+Video)

Kocha wa Al Ahly raia wa Afrika Kusini, Pitso Mosimane amesema kuwa kilichowafanya wapoteze dhidi ya Simba SC ni kutokana na hali ya joto la jiji la Dar es Salaam.

Pitso Mosimane amelalamikia hali ya hewa kuwa kikwazo kikubwa kwenye mchezo wao dhidi ya wenyeji Simba kwenye michuano hiyo ya Caf Champions League.

Miamba hiyo ya Afrika ilikubali kipigo cha goli 1-0 katika mchezo huo wa Group A katika uwanja wa Mkapa ambao umeshuhudiwa na mashabiki elfu 30,000.

Winga raia wa Msumbiji, Luis Miquissone akiwa ndiye muuaji wa Al Ahly baada ya kupigwa gonga gonga kadhaa kati yake na kiungo Clatous Chama kabla mpira kuingia wavuni ukimuacha mlindalango wa Al Ahly, Mohamed El Shenawy akishindo kuuokoa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents