
Real Madrid inadaiwa kumfikiria Mchezaji wa Manchester City, Julian Alvarez kama mbadala wa Kylian Mbappe endapo watashindwa kumsajili staa huyo wa PSG dirisha lijalo la usajili.
Licha ya kuwa Mbappe atasalia kama chaguo namba moja, lakini Madrid imempendekeza Mshambuliaji huyo wa City kama mbadala.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa akianza kwenye mechi za hivi karibuni na kubahatika kuifungia Man City magoli.