Habari

Julieth Lugembe arejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki

MWANASIASA Queen Julieth Lugembe amerejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi- CUF katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kurejesha fomu hiyo, Julieth alisema kuwa anaomba ridhaa ya chama kumchagua kuwania nafasi hiyo kutokana na kuwa anaweza kusaidia kuleta maendeleo ya chama na taifa kwa ujumla.

Alisema,”hii ni nafasi adhimu na yenye tija kubwa kwa mustakabali wa CUF na taifa letu kwa ujumla zipo sababu nyingi zilizonihamasisha kupigania Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki kupitia chama cha CUF ambacho ni makini chenye shauku ya kuwainua watanzania ndani na nje ya nchi, nina imani kuwa kitanichagua kwenda katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ili nako nipitishwe kwenda Bunge la EAC ili sasa nikapiganie mustakabali wa nchi na CUF kwa ujumla.

Nigusie yale ambayo CUF itanufaika nayo ili ikibidi nipitishwe kwenda kuingia hatua ya pili, nitahakikisha kuwa CUF inazidi kuboresheka zaidi hususan kwa kukiongezea uimara wake kwa kukijengea ofisi kadhaa ambazo zitakuwa kiungo zaidi katika kuimarisha siasa za chama.

Sitoishia hapo bali nitakiwezesha kifanyaje shughuli zake kiufanisi zaidi kwa kuboresha vitendea kazi kwa watendaji wa chama na kushiriki katika kujenga mkakati wa kuwavuta zaidi vijana na kuwajengea uwezo wa kisiasa wanachama wanawake.

Related Articles

Back to top button