Habari

Julio aanza kuwakataa Singida FG

Kocha wa Singida Fountain Gate, Jamhuri Kihwelo (Julio) amesema hajajua hatma yake ndani ya kikosi chake na anataka kuzungumza na Rais wa timu hiyo Japhet Makao ili kujua hatma yake kikosini humo.

Kocha huyo hivi sasa yuko zake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya sikukuu na kikosi hicho kipo kipo chini ya Kocha msaidizi Ngawina Ngawina.

Julio anasema “Nimekuja nyumbani kula sikukuu na familia yangu na timu iko chini ya msaidizi wangu, kuna vitu haviko sawa nasubiri kukutana na Rais ambaye alikuwa Afrika Kusini tuzungumze na mambo yakienda sawa nitabakia”

Julio aliyeinusuru KMC kushuka msimu uliopita amesema makocha wa kitanzania wanaonekana hawawezi, lakini makocha kutoka nje wanathaminiwa.

“Mimi ni kama Mpalestina sitaki kusifiwa najisifia mwenyewe, lakini makocha wa kitanzania tunakutana na changamoto ndani ya soka letu”.

“Akija kocha Mzungu na kuna vitu akisema haraka vitu hivyo vinafanyika lakini akija Julio au Kocha mwingine wa ndani anaonekana haiwezekani” alisema Julio.

 

 

 

 

 

 

 

 

CHANZO: WASAFI FM, SPORT ARENA.

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents