Habari

Justin Bieber amepona tatizo lake la kupooza

Miezi chache tu baada ya Justin Bieber kulazimika kusitisha Tamasha lake ya dunia kwenye baadhi ya mataifa yaliyokuwa yamesalia baada ya kuingiwa na wasiwasi wa kiafya uliotokana na kugunduliwa kwake na ugonjwa wa Ramsay Hunt Syndrome,ambapo aliparalaizi sehemu moja ya mwili wake mwimbaji huyo tayari yuko katika hali nzuri zaid.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alitangaza mnamo Juni 2022 kwamba aligunduliwa na ugonjwa wa Ramsay Hunt Syndrome 2, ambapo alisema kuwa upannde mmoja wa mwili wake haufanyi kazi umeparalaizi kuanzia kwenye jicho, mdomo na mkonno mmoja.

Baada ya mashabiki kuuliza maswali mengi juu ya ukimya wake na je afya yake, siku ya jana Justinn aliamua kuweka video kwenye insta story yake na kuweka sura yake huku akitabasamu kwa furaha.

Video hiyo ni ishara kuwa yupo mzima wa afya na amepona tatizo lake hata jicho lake linafanya kazi vuzuri.

Picha ya kwanza akicheka baada ya kupona na picha ya pili akionyesha tatizo lilivyoanza

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents