Umbea

Kajala na Harmonize wameachana ? afuta picha za Harmonize Instagram na kumu – unfollow

Moja kati ya taarifa inayo-trend kwa sasa mitandaoni ni kuhusu msanii wa filamu Kajala Masanja na msanii wa muziki Harmonize ambao inasemekana penzi lao limefika mwisho kutokana na baadhi ya viashiria vya mazingira vilivyojitokeza.

Taarifa hiyo imekuja baada ya Kajala Masanja kufuta picha zote alizowahi ku-post akiwa na Harmonize kwenye mtandao wa Instagram kisha kumu-unfollow kwenye mtandao na kuandika ujumbe wa Kiingereza uliotafsirika kama

Usimuumize mtu kwa ajili ya sababu zako binafsi

Mahusiano ya Harmonize na Kajala yalikuja kwa kasi na yalivutia watu wengi hadi kufikia hatua ya kuchorana tattoo japo baadhi ya watu wengine walikuwa wanalipinga penzi lao mitandaoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents