Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Kipi bora msanii kufanya kiki au kutofanya kiki kabisa??

Kupitia kipindi cha RECAP na MANDO @el_mando_tz leo amezungumzia kitu kingine kabisa, amezungumzoia namna kiki zinavyosaidia kukuza majina ya wasanii na kuwafanya wauze bidhaa zao (nyimbo/muziki) kwa uarahisi zaidi.

Ameongeza kuwa msanii anapozungumziwa haijalisha kwa uzuri au kwa ubaya itamsaidia kumtangaza katika jamii na hapo wale ambao walikuwa hawamjui wataanza kumfuatilia na kufuatilia kazi anazofanya.

@el_mando_tz ameongeza Muziki wa sasa hivi kwa kizazi hiki ni biashara na hakuna biashara yoyote innayoweza kufanikiwa bila matangazo, kwa upande wa wasanii matangazo yao ya kutangaza kazi zao kwa asilimia kubwa ni kuzungumziwa.

Msanii atazungumziwa vipi ni pale annapotoa wimbo mzuri au kufanya jambo fulani (Kiki) ili watu wamzunngumzie, msanii atafanikiwa kuuza muziki wake bila kujali amezungumziwa kwa mazuri au mabaya.

Kinachotakiwa kuzingatiwa ni kwamba msanii wafanye kiki ambayo haitashusha brand yake bali afanye kiki ambayo itamfanya azungumziwe tu.

Ndio maanna akina Diamond, Alikiba, Harmonize, Rayvanny na wengine wannafanya vizuri sana kwenye muziki huu kwa sababu kila siku hawaishiwi matukio na hayo matukio ndio yanafanya watu wafuatilie muziki wao.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents