Habari

Kama Ndoto! Secilia Akabidhiwa Magari Mawili Aliyojishindia Magifti Dabodabo, Moja Ampa Dada Yake

Neema Ndunguru (katikati) akipokea mfano wa funguo ya gari kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo Edwardina Mgendi wapili kutoka kulia na Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha kulia. Kushoto kukiwa na wahamasishaji wa Kampeni ya Magifti Dabodabo Hamisa Mobetto kushoto na Haji Manara.

Dar es Salaam 15 Februari 2024: Kampeni ya Magifti Dabodabo iliyoanza Novemba mwaka jana leo imehitimishwa kwa kumkabidhi mshindi wa zawadi ya gari, Secilia Ndunguru ambaye alipewa magari mawili.

Mshindi huyo ambaye hakuwepo eneo la tukio kutokana na changamoto ya kiafya gari gari lake alikabidhiwa mwakilishi wake ambaye ni mdogo wake Neema Ndunguru na gari la mshindi mwenza alikabidhiwa dada yake Jacqueline Ndunguru ambaye mshindi huyo alimchagua kuwa mpendwa wake aliyependa naye ‘agiftishwe’ gari hilo.

Mshindi mwenza aliyechaguliwa na mdogo wake kushinda naye, Jacqueline Ndunguru akifurahia gari alilopewa na Secilia.
Magari hayo walikabidhiwa na Semaji la promosheni hiyo Haji Manara aliyekuwa na mhamasishaji wa kampeni hiyo, Hamisa Mobetto huku Tigo wakiwakilishwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, Edwardina Mgendi na Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha.

Baada ya kukabidhi magari hayo Edwardina alielezea jinsi kampeni hiyo ilivyobadilisha maisha ya wateja wa Tigo kwa kuwazawadia vitu mbalimbali kama vile vifaa vya ndani vya kielekroniki kutoka Kampuni Hisense, pesa taslimu, muda wa maongezi na vinginevyo.

Kwa upande wake mshamasishaji wa kampeni hiyo Hamisa Mobetto baada ya kumpongeza Secilia kwa ushindi huo alisema anajisikia fahari sana kufanyakazi na Tigo kwa jinsi inavyotoa huduma bora kwa watumiaji wake na kubadilisha maisha yao kwa kampeni mbalimbali kama hiyo.

Semaji la kampeni hiyo, Haji Manara naye aliisifu kampuni kwa huduma zake na kukumbushia alivyokuwa mbugani huku akifurahia mtandao wenye kasi wa kampuni hiyo.

Katika shukrani zake Neema ambaye alimuwakilisha dada yake amesema tukio hilo limekuwa kama ndoto maishani mwao kwani hapo awali hawakuweza kuamini mpaka walivyoona jina la dada yake huyo Secilia likipostiwa kwenye kurasa za Tigo na Semaji la kampene hiyo, Haji Manara ndipo walipoanza kuamini. Neema aliwasihi watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Tigo kwani mambo yao siyo ya kubahatisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents