HabariMichezo

Kama ufurahishwa namna tunavyocheza usiagalie mechi zetu – Kocha Ufaransa

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anasema watu ambao wamechoshwa na mtindo wa uchezaji wa timu yake wanaweza kutazama kitu kingine badala ya nusu fainali ya Euro 2024 Jumanne dhidi ya Uhispania.

Les Bleus imekosolewa na baadhi ya watu kwa kukosa kuburudisha katika mechi zao, huku mchambuzi wa BBC na mshambuliaji wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Chris Sutton wiki iliyopita akisema “angefunga pazia” iwapo Ufaransa ingekuwa inacheza katika bustani yake ya nyumbani .

Haya yanajiri baada ya Ufaransa kutinga hatua ya nne bora ya michuano hiyo nchini Ujerumani huku ikiwa hakuna mchezaji wao aliyefunga bao katika mchezo wa wazi.

Mabao yao matatu kwenye michuano ya Euro yamekuwa mawili ya kujifunga wenyewe na penalti iliyofungwa na Kylian Mbappe katika sare ya 1-1 dhidi ya Poland katika hatua ya makundi.

Katika mkutano wa wanahabari wa Jumatatu kabla ya mechi, Deschamps aliulizwa kuhusu kucheza “soka inayochosha” na mwandishi mmoja wa habari, ambapo alijibu: “Ikiwa umechoshwa, tazama mchezo mwingine – sio lazima utuangalie, ni sawa.

“Labda sio sawa na ilivyokuwa zamani, lakini tuna uwezo wa kuzua hisia na kuwafanya wanaume na wanawake wengi wa Ufaransa kufurahishwa na matokeo yetu, haswa baada ya kipindi kigumu katika nchi yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents