Habari

Kamati Kuu ya CCM yaja na maadhimio haya

Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kimefanyika jana Novemba 05, 2025, jijini Dodoma.

Hicho ni kikao cha kwanza kufanyika tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mfunzo wa chama hicho, Kenani Kihongozi amesema pamoja na mambo mengine, kikao hicho maalumu kilitafakari hali ya kisiasa nchini kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 na kuazimia mambo kadhaa.

Amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imewapongeza kwa dhati wananchi wote wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kuonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Kihongozi amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa inalaani vitendo vya kihuni na uvunjifu wa amani vilivyofanywa na baadhi ya watu, vilivyosababisha vifo na uharibifu wa mali za umma na za wananchi.

“Chama Cha Mapinduzi kinaazimia kujitathimini na kujipanga vyema kubeba dhima ya kuliongoza Taifa pia kinaitaka Serikali kuchukua hatua muafaka za kuhakikisha nchi inabaki katika hali ya amani na utulivu,” amesema Kihongosi

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents