Habari

Kampuni ya Silverlands Tanzania miongoni mwa kampuni zinazokuwa kwa kasi Afrika

Ripoti ya utafiti ya ‘Financial Times’ imeitaja Kampuni ya Silverlands Tanzania kuwa ni miongoni mwa kampuni zinazokuwa kwa kasi barani Afrika.

Ripoti hiyo imezitaja jumla ya kampuni bora 75 barani Afrika kwa kuzingatia vigezo vya ukuaji mkubwa wa mapato kati ya mwaka 2017 na 2020.

Kampuni sita tu katika sekta ya kilimo ziliweza kuwa miongoni mwa kampuni hizo 75.

Kampuni ya Silverlands ni miongoni mwa kampuni mbili tu za Kitanzania zilizofanikiwa kuwa miongoni mwa kampuni bora 75 kwa kufanikiwa kuwa na ongezeo la mapato yake kwa asilimia 40.4, na hivyo kushika nafasi ya 25 kwenye nafasi hizo 75.

Kampuni imefanikiwa kukua kwa kiwango hicho hata katika kipindi kigumu cha athari za ugonjwa wa Uviko-19.

Kampuni ya Silver Street Capital, ambayo ni mshauri mkubwa wa masuala uwekezaji, kwa mara ya kwanza iliwekeza katika kampuni Silverlands Tanzania mnamo mwaka 2014 kwa dhumuni la kuleta matokeo chanya katika wafugaji wadogo wa kuku na wakulima wa nafaka katika nchi za Afrika Mashariki, sekta ambayo huko nyuma ilikuwa ina maendeleo ya kiwango cha chini.

Kampuni ya Silverlands Tanzania imejikita kwenye biashara ya kuku na kuzalisha vyakula na vifaranga vyenye ubora wa hali ya juu.

Kutoka mwaka 2014 mpaka sasa, Silverlands Tanzania imekua ni Kampuni yenye uzalishaji mkubwa wa vyakula vya kuku Tanzania na pia ni ya tatu kwa uzalishaji wa vifaranga vya siku, ambapo iliuza vifaranga milioni 14 mwaka 2021.

Kabla ya Silverlands, sekta ya ufugaji kuku ilibaki kuwa ya chini kwa sababu ya kukosekana vifaranga vya kutosha na vyenye ubora.
Kampuni ya STL ilianzisha aina mpya ya kuku wa kisasa wa ‘layers’ na ‘broilers’ vile vile ‘Sasso’.

Hatua hiyo ni katika kuleta aina ya kuku wa kisasa wanaofaa kwa mazingira ya vijijini.

Kuku na chakula kinachozalishwa na Silverlands Tanzania kinalewalenga wafugaji wadogo ambao huwakilisha kundi kubwa la wafugaji hapa Tanzania.

Kwa chakula bora na vifaranga, wafugaji wa kuku wanaweza kuzalisha kuku kwa faida na uhitaji umekuwa ukikua.

Kuongezeka kwa uzalishaji wa kuku na mayai kumesaidia kupunguza kwa utapio mlo kwa watoto, tatizo ambalo limeenea katika nchi za Kusini mwa Afrika.

Kampuni ya Silverlands Tanzania ilianzisha kiwanda cha kwanza cha kuchakata soya na hii imesaidia kufanya maharage ya soya kuwa kwenye mzunguko na mahindi kwa wazalishaji wadogo wa nafaka kuongeza upatikanaji kutoka hali ya awali.

Kampuni ya Silverlands Tanzania kwa sasa inanunua mahindi na soya kutoka kwa wakulima wadogo 29,000.

Kampuni ilianzisha na kuendesha vituo 19 vya usambazaji nchini kote vikiwa na wasambazaji wadogo wadogo wapatao 350 wanaouza bidhaa zake kwa wafugaji wadogo wa kuku wapatao134,000, ambao asilimia 75 ni wanawake.

Kipato cha wakulima hao wadogo kimeongezeka kwa asilimia 50 kwa sababu ya kampuni ya Silverlands Tanzania.

“Tunajisikia faraja kwa ukuaji mkubwa wa kampuni ya Silverlands Tanzania nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Imeonesha ni kwa namna gani biashara inaweza kutengenezwa kwa faida, kukua kwa kasi na kuwa na matoeko chanya katika jamii kwa kukuza vipato vya maelfu ya wakulima wadogo,” Dk Ben Moshi, mwenyekiti wa Silverlands Tanzania Limited, amesema.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa uwekezaji wa kampuni ya SilverStreet Capital, Bw Gary Vaughan-Smith, amesema: “ Uongozi wa Silverland Tanzania umefanya kazi ya kipekee kwa kuanzisha biashara yenye nguvu yenye ukuaji mkubwa nchini Tanzania, japokuwa kuna ugonjwa wa Uviko-19.

Biashara inaleta manufaa makubwa kwa jamii kwa sababu bidhaa zake zimejikita kwenye kuboresha hali za wakulima wadogo kwa kuwaletea faida.

Ni mfano mzuri wa kuigwa katika ukanda wa kusini mwa Afrika kwa kuonesha namna gani unaweza kuwekeza kwa mafanikio na kuleta mabadiliko katika jamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents