Habari

Kanali Assimi Goita aapishwa kuwa Rais Mali

Kiongozi wa Mali Kanali Assimi Goita ameahidi kutimiza ahadi za nchi yake na kusisitiza lengo la kuandaa uchaguzi kufikia Februari mwakani, baada ya kuapishwa kuwa rais wa mpito, kufuatia mapinduzi yake ya pili katika muda wa chini ya mwaka mmoja.

Mali :Assimi Goïta afanya Mapinduzi ya pili ya kijeshi chini ya mwaka mmoja  - BBC News Swahili

”Hali hii mpya inatupa fursa ya kuurejesha mchakato wa mpito kwenye njia katika mwelekeo wanaoutaka watu. Changamoto ni nyingi, matarajio halali ya watu ni makubwa. Hata hivyo, tunapaswa kuimarisha uthabiti wetu na matumaini yetu ya maisha bora.

Huu ndiyo wajibu wangu kama mkuu wa nchi na naelewa ukubwa wa jukumu hili,” alisema Kanali Goita. Sherehe hiyo iliyofuatiliwa kwa karibu mjini Bamako imejiri baada ya Goita, ambaye aliongoza mapinduzi Agosti mwaka jana, kumuondoa madarakani rais wa kiraia na waziri mkuu wa serikali ya mpito Mei 24.

Kwa kufanya hivyo, alisababisha makelele ya kidiplomasia na kuongeza hofu ya kuzuka machafuko katika taifa ambalo ni muhimu kwa juhudi za kupambana na uasi wa makundi ya Kiislamu unaosambaa katika kanda ya Sahel.

Goita amechukuwa nafasi ya Bah Ndaw, amabye alimlazimisha kuachia madaraka mwezi uliyopita, pamoja na waziri mkuu, Moctar Ouane.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents